The House of Favourite Newspapers

Soko la Usafiri wa Kukodi Liko Katika Nafasi ya Kukua Ukanda wa Afrika Mashariki

0

Sekta ya usafirishaji imekuwa kwa haraka katika nchi nyingi barani Afrika kutokana na kuwepo kwa usafiri wa kukodi ambako wateja wanatafuta kupata usafiri salama na wenye gharama nafuu.

 

Kanda ya Afrika Mashariki vile vile unashuhudia kukua kwa usafiri wa kukodi ambapo huduma mbalimbali kama vile Bolt wanatoa huduma kupitia katika mfumo wao uliyopo katika application yasimu. Soko la kukodi usafiri kwanjia ya mtandao (E-hailing Market) katika Afrika na Mashariki  ya Kati lilitazamiwa kukua kufikia Dola bilioni 7.3 kufikia mwaka 2023.

 

 

Sababu kubwa zinazochochea kuwepo kwa mahitaji ya usafiri wa kukodi katika kanda hii ni pamoja na kukua kwa miji, ongezeko la idadi ya vijana, kuongezeka kwa uwekezaji unaofanywa na watoa huduma za usafiri wa kukodi na ongezeko la idadi ya watumiaji wa simujanja (smartphone)na mtandao wa internet.

 

 

Tanzania haiko tofauti na nchi nyingine, kutokana na ongezeko la watumiaji wa mtandao wa internet na smartphone, watu katika miji na majiji kama vile Dar es salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha wanapata fursa ya kufurahia huduma ya usafiri wa kukodi ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika namna ambavyo watu wa mijini wanavyosafiri.

 

 

Akitoa maoni kuhusu maendeleo ya huduma ya usafiri wa kukodi katika soko la ndani, Maneja wa Bolt Tanzania, Remmy Eseka amesema kwamba huduma ya usafiri wa kukodi unashuhudia ukuaji mzuri.

 

 

“Mfumo wa usafiri wa kukodi kuendana na  mahitaji wa Bolt unatoa njia rahisi na salama ya uombaji wa usafiri pale unapohitajika jambo ambalo linalowezesha watumiaji kujipatia usafiri kama wanavyohitaji na kwa gharama nafuu.

 

 

Huduma zetu zinahakikisha kwamba wateja wanaweza kufahamu kwausahihi niwapi gari lilipo, wanaweza kufuatilia safari zao na wanaweza kuchukuliwa na kushushwa mahali popote wanapohitaji, jambo linalopelekea huduma zetu kuongezeka umaarufu,” RemmyEseka, Manejawa Bolt amebainisha mambo haya kuwa ndio sababu kuu ya ukuaji imara wa kampuni yake.

 

 

Kwa kuongezea, urahisi wa kuagiza usafiri na faraja anayopata abiria kutokana na huduma ya kukodi usafiri kulingana na mahitaji unaweza kuchochea ukuaji zaidi katika tasnia ya usafiri wa kukodi Afrika hapo baadae.

 

 

“Bolt vile vile inachangia katika kukua kwa “Uchumi wa madereva” ambapo tunatoa mfumo wa Bolt kama chanzo kikuu na wakati mwingine kama chanzo cha ziada cha kiuchumi kwa madereva ambao wanataka kutekeleza majukumu mengine na wakati huohuo wakiwa wanaweza kuhudumia maisha yao.

 

 

Mfumo huu umewasaidia madereva kuwa na uwezo kamili wa kuutawala muda wao na kiwango cha fedha ambacho wanaweza kujipatia,  AlihitimishaEseka.

 

 

Mwaka 2017, shirika la Global Sachs lilitabiri kuwa miaka 10 ijayo itakuwa na mabadiliko makubwa zaidi katika jinsi ambavyo watu na bidhaa wanavyosafiri kuliko ilivyokuwa katika miongo mingine tangu kuvumbuliwa kwa vyombo vya usafirishaji.

 

 

Kadri ambavyo dunia inajitahidi kukabiliana na kujifunza kuishi na janga la Covid-19, teknolojia mpya zinazochipukia na mifumo ya biashara kama usafiri wa kukodi, magari yanayojiendesha  yenyewe na huduma ya usafirishaji wa mizigo, vyombo vya usafiri vya kukodi na hatae VTOL (magari yanayoruka) yanachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha faida katika huduma ya usafirishaji ambayo kituo cha utafiti cha Goldman Sachs Research kimekadiria kuwa kitazidi dola bilioni 700.

Leave A Reply