Soma Hapa CV ya C.E.O Mpya wa Simba, Barbara

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (C.E.O), Barbara Gonzalez Septemba 7, 2020 alichaguliwa na Bodi ya Wakurugenzi kuchukua nafasi iliyoachwa na Senzo Mazingisa ambaye kwa sasa anafanya kazi ndani ya Klabu ya Yanga akiwa ni mshauri mkuu kuelekea kwenye masuala ya mabadiliko ya klabu hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohamed Dewji, amesema: “Hatujakurupuka kufanya maamuzi wala sio maamuzi yangu, ni ya kikao kwani tulikaa jana (juzi) na kuamua kumpitisha Barbara, anakuwa CEO wa kwanza mwanamke. Ni mchapakazi na anaipenda Simba, hivyo tunaamini kila kitu kitakwenda sawa.”

 

Akizungumza baada ya uteuzi huo, Barbara alisema: “Mimi sio muongeaji sana ila ninawaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.”

Toa comment