The House of Favourite Newspapers

Songea: Mwanafunzi Kidato cha Tano Ajinyonga

0

WANAFUNZI wa kidato cha tano anayesoma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana St. Agness Peramiho, Sophia Joel Mbano (19) amekutwa amefariki Dunia kwa kujinyonga juu ya mti kwa kumtumia kamba iliyodaiwa kuwa ya Manila.

 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa amesema kuwa tukio hilo limetokea Mei 18 mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana huko katika pori linalomilikiwa na Seminari Kuu ya Peramiho katika Kitongoji cha Amani Kata ya Peramiho Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

 

Alisema kuwa mpaka sasa chanzo cha tukio bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea huku akitoa rai kwa wazazi, walimu na walezi kuhakikisha wanawafuatilia kwa ukaribu wanafunzi ili kubaini matatizo yanayo wakabili.

Leave A Reply