Kartra

Yanga Yawapigisha Kwata Maafande wa JKT, Yawapiga 2 – 0

TIMU ya JKT Tanzania imeshindwa kufurukuta baada ya kuchapwa na Yanga kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mchezo uliochezwa leo Mei 19, 2021 kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 

Yanga ambao walionekana kucheza vizuri kipindi cha kwanza walifanikiwa kupachika bao la kuongoza kupitia kwa Yacouba Sogne dakika ya 27 ya mchezo.

 

Dakika mbili baadae wanajangwani walifanikiwa kuzifumania nyavu za JKT, kupitia kwa Tuisila Kisinda.

Kipindi cha pili JKT walionekana kucheza vizuri zaidi lakini hawakufanikiwa kupata goli.

 

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 61 sawa na watani zao wa jadi Simba na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa.

 

 


Toa comment