The House of Favourite Newspapers

SERENA WILLIAMS KULIPA FAINI MIL. 8 KWA KUVUNJA SHERIA

NYOTA wa mchezo wa tenisi, Mmarekani, Serena Williams, amepigwa faini ya Dola 17,000 kwa kukiuka sheria za mchezo huo wakati wa pambano lake na Naomi Osaka, Jumamosi iliyopita nchini Marekai.

 

Mrembo huyo mweusi, alipigwa faini ya Dola 4,000 kwa kukiuka utaratibu wa kupewa mafunzo ya mchezo huyo na kocha wake, Dola 3,000  kwa kubamiza ovyo raketi yake, na Dola 10,000 kwa kutoa lugha mbaya kwa mwamuzi.

Fedha hiyo itakatwa kutoka Dola mil. 1.85 alizopata kutokana na mchezo huo ambapo Osaka alitwaa kombe la ushindi licha ya Serena kulalamika kuonewa.

Comments are closed.