The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai Azindua Kitabu cha Ugonjwa wa Kisukari

0
Dk. Sadick Sizya (kulia) akimkabidhi Spika wa Bunge Job Ndugai (katikati) kitabu kilichosheheni maelezo kuhusu ugonjwa wa kisukari. Kulia ni Nestory J Enyas kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili.

SPIKA wa bunge Job Ndugai amezindua rasmi kitabu cha ‘UGONJWA WA KISUKARI NA SULIHISHO LAKE ‘chenye lengo la kuelimisha umma kuhusu ugonjwa huo.

 

Kitabu hicho kimeandikwa na Dk. Sadick Sizya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Afisa muuguzi wa hospitali hiyo Nestory J Enyas.

 

NdugaiĀ  amezindua kitabu hicho jana Januari 29, 2020 nje kidogo ya ofisi kuu za Bunge zilizopo jijini Dodoma.

 

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Ndugai alitoa wito kwa Watanzania kusoma kitabu hicho ili kupata maarifa namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

 

Aidha, Dk. Sizya ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya habari za afya, alisema wameona umuhimh wa kuandika kitabu hicho ili kuiwezesha jamii kupata maarifa namna ya kubadilisha mtindo wa maisha ili kuzuia ugonjwa huo.

 

“Ugonjwa huu wa kisukari umekuwa tishio kubwa sana kwa jamii maana sasa si ugonjwa aa matajiri wala watu wenye umri mkubwa, hata watoto umewaathiri hali tunayoona kuna umuhimu wa jamij kubadilisha style ya maisha,” alisema.

Na Mwandishi wetu

Leave A Reply