The House of Favourite Newspapers

Spika wa Bunge Akutana na Viongozi wa TFF

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirikisho hilo, Ndg. Mohamed Abdulaziz katika Ofisi yake iliyopo Bungeni Jijini Dodoma leo Februari 10, 2022.

 

Katika Mazungumzo yao, Dkt. Tulia ambaye pia ni Mjumbe wa bodi hiyo, amewaahidi Viongozi hao kuendeleza ushikamano wa dhati baina yao na taasisi ya Bunge katika kuongeza chachu ya mafanikio katika sekta ya michezo nchini.

“Kwanza niwashukuru sana Viongozi wangu kwa kuweza kunitembelea, hii inaonesha ni kwa namna gani mnaithamini taasisi yetu. Kikubwa zaidi niwaahidi tu ya kwamba sisi kama Bunge tutaendelea kutoa ushirikiano wote utakaohitajika kwa lengo la kuhakikisha tunakuza na kuboresha sekta ya michezo nchini” alisema Spika Dkt.Tulia

Na kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirikisho hilo, Ndg. Mohamed Abdulaziz, amemshukuru Spika Dkt. Tulia Ackson kwa mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa katika sekta ya michezo na kusema kwamba amekuwa mfano bora wa viongozi.

Leave A Reply