The House of Favourite Newspapers

Sportpesa Bet Bonanza Kutoa Kitita cha Shilingi Milioni 15.8 Wiki Ijayo

0
   Promosheni inaendelea mpaka wiki ijayo April 12 ambapo zawadi ya Tsh. 15,888,000 itatoka kwa mshindi wa jumla

WASHINDI watatu, Shaaban Mwita wa Mgusu, Geita, Abdalla Said Ali wa Tandahimba, Mtwara na David Jonas wa Magu, Mwanza, leo asubuhi wameibuka washindi wa vitita vya shilingi milioni moja moja kila mmoja katika droo ya nne ya wiki ya Bet Bonanza ya Sportpesa.

Droo hiyo ni sehemu ya promosheni ya Bet Bonanza ya Sportpesa, na pia ni muendelezo wa zawadi ambazo zinatolewa katika kipindi hiki cha ligi mbali zinazoendelea kwa ushirikiano na kampuni za simu Airtel, Vodacom na Halotel.

Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa makao makuu ya Sportpesa jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Sportpesa, Sabrina Msuya amesema leo imechezeshwa droo ya nne katika wiki ya nne ya Bet Bonanza ambapo wateja wa Halotel, Airtel na Vodacom wameshinda vitita hivyo vya shilingi milioni moja moja kwa kila mmoja.

 

“Katika mwendelezo wa kampeni yetu ya Bet Bonanza, muda mfupi uliopita imechezeshwa droo ya nne ya wiki ya Bet Bonanza ambapo wateja watatu kutoka Geita, Mtwara, Songwe na Mbeya, wameshinda shilingi milioni moja moja, baada ya kubashiri na kuibuka washindi wa Bet Bonanza ya Sportpesa.

 

“Napenda kuwapa kongole washindi wetu wa leo na pia kuwapa moyo wachezaji ambao wameshiriki na hawakushinda wasikate tamaa kwani promosheni bado inaendelea mpaka wiki ijayo April 12 ambapo ile droo kubwa kabisa ya kufunga kampeni ya Bet Bonanza itafanyika, ambapo zawadi ya Tsh. 15,888,000 itatoka.

Akiongea baada ya droo hiyo ya shilingi milioni moja moja kwa kila mtandao, Afisa Biashara kutoka Vodacom, Karen Samson amempongeza mshindi Shaaban Mwita kwa kushinda milioni moja na kuwaasa watumiaji wa Vodacom kuendelea kubashiri na Sportpesa kupitia Bet Bonanza ili waingie kwenye droo kubwa ya mwisho ya Tsh. 15,888,000 jumanne wiki ijayo.’’

“Ni matumaini yangu mtachangamkia fursa ya Bet Bonanza. Kuweka pesa kwa Mpesa bofya *150*00#, Chagua 4 – Lipa bili alafu fuata maelekezo.”

Naye Afisa biashara kutoka Halotel, Roxana Kadio alimpongeza mshindi Abdalla Said Ali kwa ushindi huo na kuwataka watumiaji wa Halotel kuendelea kucheza na Sportpesa kupitia Bet Bonanza ili waingie kwenye droo kubwa ya Jumanne Tarehe 12 ili waweze kujishindia Tsh. 15,888,000.

‘’Ninawaomba wateja wetu wa Halotel wajitahidi kucheza kuanzia leo na kuendelea kwani Jumanne ya wiki ijayo promosheni hii ya Bet Bonanza inafika mwisho na ile zawadi kubwa kabisa ya Tsh. 15,888,000 itatolewa, hivyo basi bado mnayo nafasi ya kushinda.

Kuweka pesa kwa halopesa piga Piga *150*88#, Chagua 4:, Lipia kwa HaloPesa, Chagua 4: Michezo ya Kubahatisha.

Promosheni hii ilizinduliwa rasmi Machi 8, 2022 na inajumuisha zawadi za shilingi elfu 20 kila siku, zawadi za milioni moja moja kwa washindi watatu kila wiki na zawadi ya milioni 15,888,000 siku ya kufunga promosheni.

Leave A Reply