The House of Favourite Newspapers

Sportpesa Yatangaza Jackpot Mpya Ya Shilingi Milioni 985

0

 

Kampuni kubwa ya michezo ya kubashiri (betting) ya SportPesa, imetangaza ‘Jackpot’ mpya ambapo sasa mshindi anaweza kujishindia mpaka shilingi 985,669,400/- kwa dau la shilingi 2000 pekee.

Akitangaza kuzinduliwa kwa Jackpot hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Abbas Tarimba, amesema Jackpot hiyo ni endelevu na mpaka sasa hakuna kampuni yoyote ya ‘betting’ nchini inayotoa dau kubwa kama hilo.

“Tunapenda kuchukua fursa hii kutoa taarifa kupitia vyombo vyote vya habari hapa nchini kwamba kwa sasa hakuna kampuni yoyote yenye dau kubwa zaidi ya hili na kumtangaza mshindi wa Jackpot kubwa kama hii, ambapo mpaka sasa hii ni mara ya tatu kwa Jackpot endelevu kupanda kwa dau zaidi ya nusu bilioni, baada ya kuanzia shilingi milioni 200.

“Kwa hakika, kiwango hiki kama hakitapata mshindi mwishoni mwa wiki hii, basi dau litakalofuata, litaweka historia ya kuwa dau la kwanza la ubashiri kufika bilioni moja kwa viwango vya Jackpot endelevu nchini,” amesema Tarimba na kuongeza:

‘’Tunapenda kuwasisitiza watanzania wote kwa jumla kucheza mara nyingi kadiri muwezavyo ili kupata nafasi kubwa ya kushinda Jackpot hii nono ambayo ilianza kushindaniwa kuanzia April, 2021 baada ya mshindi wa 7 wa Jackpot, Abdulaziz Ngamilo kupatikana.

“Jambo jema na zuri kwa wachezaji ni kwamba hata kama hukufanikiwa kushinda dau hili moja kwa moja, una nafasi nyingine ya kushinda kupitia Jackpot bonasi kwa washindi wanaopatia kuanzia timu 10,11 na 12”
Tangu kuanza kwa Jackpot hii karibu miezi 11 Iliyopita, SportPesa imeshatoa washindi wa Kitanzania zaidi ya 200 kila wiki kwa waliobashiri kwa usahihi kuanzia mechi 10, 11 na 12.

“Washindi wa SportPesa Jackpot kwa mara ya kwanza walipatikana Agosti, 2019 Agosti ambapo Magabe Marwa na Kingsley Pascal waligawana kiasi cha shilingi 825,913,864 baada ya Jackpot hii kukaa kwa miaka miwili.

“Kwa mara ya pili na tatu walipatikana washindi wengine ambao ni Scolastika Ngwaluweson na Jamal Khalfan Abdallah ambapo waliondoka na kiasi cha shilingi 260,319,980 na 288,974,720.

“Washindi waliofuatia ni Lilian Laizer na Yassini Ridhiwani ambao walijishindia shilingi 267,800,060 na 437,631,320,” alisema Tarimba.

Kwa upande wake, Meneja wa Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya ameongezea kuhusiana na dau hilo na namna ya kushinda huku akiwataka Watanzania kuchangamkia fursa bila kusita wala kuwa na visingizio ili kuwa mabilionea.

‘’Jackpot ndio njia rahisi kabisa ya kuwa bilionea ajae kwa kufuata taratibu nyepesi za uchezaji, kwa kutumia mitandao yetu ya kijamii na tovuti yetu ya www.sportpesa.co.tz, App ya sportpesa na USSD (*150*87#),” alisema

Leave A Reply