The House of Favourite Newspapers

Staa Bongo Muvi Mbaroni kwa Ubakaji

0

MSALA! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia, msanii wa Bongo Muvi; Hussein Mbega ‘Niva’ kuswekwa ndani kwa msala wa ubakaji na wizi ambapo jalada la kesi aliyofunguliwa inasomeka; OB/IR/9494/2019 KUBAKA/WIZI, Risasi Jumamosi lina full stori. 

 

Msanii huyo anadaiwa kumbaka, mwanamke wa Kibongo anayeishi nchini Uingereza anayefahamika kwa jina la Mbuta Nanga.

 

TUMSIKILIZE MLALAMIKAJI

Akizungumza na Risasi Jumamosi akiwa kwenye kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar; Mbuta Nanga alieleza kwa undani jinsi alivyokutana na Niva hadi kufikia hatua ya kutendewa tukio hilo.

 

Alisema, aliingia jijini Dar Disemba 20, mwaka jana akitokea London anakoishi na kufikia kwenye hoteli moja iliyopo Mbezi Beach kisha akaenda kukutana na muigizaji Esha Buheti ambaye ndiye alikuwa sababu ya yeye kuonana na Niva.

“Nilienda kwa Esha sababu ni mtu ambaye tunafahamiana kabla. Nilipofika pale ndipo nilipokutana na Niva. Esha alinitambulisha na kwa kweli aliingia kwa gia kama ya kunihitaji kimapenzi, ikabidi nimuulize Esha kwamba ni mtu mzuri? Esha akaniambia kuwa ni mtu mzuri,” alisema Mbuta Nanga.

 

WABADILISHANA NAMBA ZA SIMU

Akizidi kusimulia, alisema walibadilishana namba na Niva baada ya kuaminishwa na Esha kwamba hana tatizo na wakaanza kuzunguka naye kwenye kumbi mbalimbali za starehe wakifanya starehe mbalimbali.

“Sikuona shida, nilikuwa nampa fedha zozote anazotaka na tulikuwa tunatumia. Ndani ya muda mfupi aliniingizia suala la kutaka kunioa, hivyo nikaona ni mtu mzuri kweli kama Esha alivyonieleza,” alisema.

 

ADAI KUBAKWA

Mbuta alisema, hiyo siku ambayo tulikuwa kwa Esha ilipofika jioni Niva akaniambia kwamba tuondoke twende sehemu moja ambapo wapo na wasanii wenzake wengine.

“Basi kwa kuwa niliaminishwa na Esha kwamba ni mtu mzuri na hana mke, nikakubali tukatoka na kwenda mpaka hiyo sehemu, tulipofika tukanywa na kula. Baadaye muda ukawa umeenda sana, akaniambia basi tulale hapahapa kwa sababu kuna sehemu nzuri ya VIP lakini ni 30000.

 

“Kweli nikatoa ile 30000 akaenda kulipia, mwisho wa siku tukaingia uko VIP ambapo kuna kitanda na vitu vingine, kwa ufupi ni chumba kilichokamilika.

 

“Sasa wakati tunaendelea kuongea mimi nikamwambia kuwa nataka kumjua zaidi, akanijibu kwamba yeye huwa habishani sana na wanawake, yeye huwa anawapiga tu (anawapiga kiutu uzima).

“Basi tukiwa tumelewa, aliniingilia kinguvu bila ridhaa yangu na nikama alikuwa ametumia dawa kwa sababu kwanza maumbile yake siyo ya kawaida hivyo nikaumia sana, nikawa nalalamika kuwa naumia lakini mwenzangu ndio akawa anakazana zaidi.

 

“Baada ya hapo kesho yake asubuhi tukaachana, mimi nikarudi hotelini nilipokuwa nimefikia na yeye akaondoka zake, basi baada ya kufika hotelini nikaendelea kuugulia maumivu makali ambapo hata kukaa ilikuwa shida.

 

Ilipofika mida f’lani hivi Niva akanifuata tena hotelini, alipoingia tu chumbani akanikuta nimevaa taulo za kike kwa sababu nilikuwa nimeumia sana. Yeye bila kujali akanitoa ile taulo akaanza tena kuniingilia kimwili kinguvu, nilijaribu kumtoa na kumwambia naumia lakini hakujali akaendelea,” alisema Mbuta.

KUHUSU WIZI

Akizungumzia jinsi alivyoibiwa, Mbuta Nanga alisema mbali na kumpa fedha kwa matumizi mbalimbali, Niva alimuomba shilingi milioni 2 kwa ajili ya kununua pete ili amvishe lakini hata hivyo hakufanya hivyo.

 

“Aliniambia kwamba ana kazi anaifanya ya kuingiza fedha, hivyo nimuazime shilingi milioni 2, akanunue pete kama ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ ila hii ya kwangu itaongezewa jiwe moja, nikampa. Sasa siku ya tukio, nikawa najiandaa saluni na wifi yangu Isha Mashauzi lakini hadi dakika za mwisho sikuona cha pete wala nini,” alisema na kuongeza:

 

“Kimsingi walinitapeli kwa kushirikiana na Esha maana hata Niva alipoingia mitini kila nilipomtafuta Esha naye hakunipa ushirikiano tena. Sasa hata Isha naye ambaye walikuwa wamesema atakuwa kama mtumbuizaji pia katika shughuli hiyo akawa hana kazi tena.”

 

ADAI KUMLIPIA MATAIRI YA GARI

Mbuta Nanga alisema mbali na fedha hizo, pia kuna siku Niva alimuomba fedha kwa ajili ya kubadili matairi ya gari yake yaliyokuwa yamechoka ambapo bila hiyana alimpa fedha zisizopungua shilingi milioni mbili.

 

“Ni kama vile alinifanyia kitu, mimi nikawa sijielewi, natoa tu hela. Wakati mwingine pia kwenye pochi yangu nilikuwa naona tu fedha zimeisha, tunaenda kwenye ATM tunatoa halafu ghafla tu sizioni tena,” alisema.

 

ATINGA POLISI

Mwanamke huyo ambaye asili yake ni Moshi, alisema baada ya kuona amepigwa changa la macho, alifika katika kituo cha Polisi Oysterbay na kumfungulia mashtaka ya UBAKAJI na WIZI ambapo aliambatana na askari kwenda kupimwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

 

“Daktari aliponipima aliniambia nimeharibika vibaya na kunilaumu kwa nini sikufika mapema kwani ilihitajika nishonwe kutokana na jinsi nilivyoharibiwa,” alisema.

NIVA AKAMATWA, APATA DHAMANA

Ilielezwa kuwa, baada ya mwanamke huyo kushtaki, Niva alikamatwa katika kituo hicho lakini hata hivyo alitoka kwa dhamana.

Mbuta Nanga alisema, Niva alipotakiwa kuripoti kituoni hapo hakufika hivyo polisi wanaendelea kumsaka kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

 

ESHA AMKANA

Akizungumza na Risasi Jumamosi, muigizaji Esha Buheti alisema hahusiki na suala la kumuunganisha Niva wala wizi huo kwa kuwa walikutana wenyewe na kuanzisha uhusiano wenyewe.

 

NIVA AGOMA KUZUNGUMZIA

Wakati tukio hilo lilipokuwa lamoto, mwanahabari wetu alimuuliza Niva kuhusiana na tukio hilo ambapo alisema hayupo tayari kulizungumzia kwani litamchafua na yeye anajiandaa kuachia kazi yake.

 

KAMANDA ATHIBITISHA

Kamanda wa Polisi Kinondoni, ACP Musa Taibu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akasema hawezi kuliongelea kwa kuwa lipo katika hatua ya uchunguzi.

Leave A Reply