The House of Favourite Newspapers

Stamina awapuuza wasanii wenzake

0

stamina
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Bonavetura Kibogo ‘Stamina’.

BAADA ya kuachia albamu yake mpya hivi karibuni, msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Bonavetura Kibogo ‘Stamina’ ameweka wazi kuwa ataendelea kuzipuuza kauli za wasanii wenzake za kusema kuwa albamu haiuzi.

Stamina ambaye ameiingiza sokoni albamu yake inayojulikana kwa jina la Mt Uluguru, alisema kauli hizo hazimuingii akilini kabisa na katika maisha yake yote ya muziki hatoacha kutoa albamu.

“Mimi huwa siangalii faida bali naangalia nini mashabiki wangu wanataka, tangu naanza kufanya muziki nilikuwa na malengo ya kutoa albamu kila kukicha, hivyo kila ninapoikamilisha moja huwa naona ndoto yangu imetimia na najiandaa kukamilisha nyingine ili nizidi kukamilisha ndoto zangu.

“Siangalii faida ya pesa sana bali naangalia ndoto zangu zinatimiaje, inilipe isinilipe mimi nafanya tu, ila uzuri mashabiki wangu wanafurahia kazi yangu,” alisema Stamina.

Leave A Reply