The House of Favourite Newspapers

Stamina Awazawadia Mashabiki Wake

0

Mkali wa mistari Kwenzi, Bonaventura Kibogo ‘Stamina’.

MKALI wa mistari Kwenzi, Bonaventura Kibogo ‘Stamina’ amewazawadia mashabiki wake wimbo ‘bonus track’ ikiwa ni kuwashukuru kwa kumfikisha alipo na kuwakumbusha historia yake ya muziki na maisha yake kabla na baada ya kutoka kwenye gemu.

Stamina ameachia wimbo huo unaokwenda kwa jina la Mr. Bonaventure wikiendi iliyopita siku ambayo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kusema kuwa anawashukuru mashabiki wake kupitia wimbo huo huku akiongeza kuwa wimbo rasmi utatoka hivi karibuni.

“Nashukuru Mungu, vyombo vya habari na mashabiki wangu, nimeutanguliza huu wimbo kwao kama ‘bonus track’ inayoelezea historia ya maisha yangu na kazi yangu. Kazi yangu official itatoka soon,” alisema Stamina.

Leave A Reply