The House of Favourite Newspapers

Stars Yapoteza Dhidi ya Tunisia

0

TIMU ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) ikiwa ugenini usiku wa kuamkia leo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Afcon 2022 zitakazofanyika nchini Cameroon.  Bao hilo lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Msakini dakika ya 18.

 

Ikiwa ipo kundi J, imebakiwa na pointi zake tatu baada ya kucheza mechi tatu na wapinzani wao  sawa na Libya na Equtorial Guinea, Tunisia wanafikisha pointi tisa kwa kuwa hawajapoteza mchezo kati ya mitatu ambayo wamecheza.

 

Akizungumza baada ya mchezo  huo kocha wa timu ya Tanzania, Etienne Ndayiragije, amesema kuwa kupoteza mchezo mbele ya Tunisia ni somo, hivyo watapambana kwenye mchezo wa marudio kupata matokeo mazuri kwenye dimba la nyumbani

 

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Jumanne Novemba 17, Uwanja wa Mkapa na mashabiki watakaoruhusiwa kuingia ni asilimia 50 ya uwezo wa uwanja ambayo itakuwa mashabiki 30,000    ikiwa ni kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona.

 

Leave A Reply