The House of Favourite Newspapers

Stewart atimkia Sauz na faili

0

Hans Mloli,
Dar es Salaam

AZAM FC inatarajia kuondoka nchini Jumatano ya keshokutwa kuelekea Afrika Kusini ‘Sauz’ kupambana na Bidvest Wits lakini kocha wa timu hiyo, Muingereza, Stewart Hall ametamba kuwa anaondoka akiwa ameshanasa siri nyingi za kiufundi za wapinzani wake hao.

Pamoja na hayo, Stewart ameliambia Championi Jumatatu kuwa anafahamu ubora wa timu hiyo inayoshikilia nafasi ya pili kwa sasa katika Ligi Kuu ya Sauz lakini amegundua silaha pekee ya kuwapunguza nguvu na pengine kuwashinda kabisa ni kupata mabao ya ugenini kabla ya mchezo wao wa hapa nyumbani.

Azam itavaana na Wits Jumamosi hii huko Sauz katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili baadaye nchini Tanzania.

“Tutakwenda kule nikiwa tayari nimeshaisoma Wits, nafahamu ni timu nzuri ikiwa ndani ya moja ya ligi bora za Afrika lakini nimefanikiwa kuona DVD zao tano pamoja na kutuma mtu akawaangalie kwenye mechi zao za ligi hivi karibuni, kwa hiyo nimeshawasoma vizuri tu,” alisema Stewart.

Leave A Reply