Straika England aukubali mziki wa Stars

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Burundi, Saido Berahino, ambaye aliwahi kuzicheza West Brom na Stoke City za Ligi Kuu England, amekubali kiwango kilichoonyeshwa na kikosi cha Taifa.

 

Stars dhidi yao. Burundi ilicheza na Stars katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na kesho Jumapili zitarudiana. Burundi wanatakiwa kushinda au kupata sare ya kuanzia mabao mawili wakati Stars inahitaji suluhu au ushindi.

 

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji, alianza maisha yake ya soka England mwaka 2009 mpaka 2019, huku akiwa amezitumikia West Brom na Stoke City.

 

Berahino aliliambia Champion Jumamosi kuwa, walicheza vizuri hususan katika kipindi cha pili lakini hawakufurahishwa na matokeo ya mchezo huo dhidi ya Stars ukizingatia wao ndiyo walikuwa nyumbani lakini wakashindwa kupata ushindi.

Mshambuliaji huyo aliongeza kuwa, mchezo wa marudiano hautakuwa rahisi kwao, kwa sababu Taifa Stars walipata bao la ugenini, lakini pia wana timu yenye wachezaji wazuri na wenye uzoefu mkubwa tofauti na kikosi chao ambacho kina wachezaji wengi ambao bado ni vijana.

“Tulicheza vizuri hususan katika kipindi cha pili ingawa hatujafurahishwa na matokeo tuliyoyapata kwenye mchezo wetu dhidi ya Taifa Stars, kwa sababu sisi tulikuwa nyumbani lakini tulishindwa kushinda.

“Lakini mchezo wa marudiano hautakuwa rahisi kwetu, kwa sababu wenzetu walipata bao la ugenini na wana wachezaji wazuri na wenye uzoefu tofauti na kikosi chetu ambacho kina wachezaji wengi vijana ila chochote kinaweza kutokea,” alisema Berahino.

Said Ally na Abdulghafal Ally (TUDARCo)


Loading...

Toa comment