The House of Favourite Newspapers

Jeshi Lazima Jaribio la Mapinduzi Sudan

JESHI  la Sudan limesema Baraza la Kijeshi la nchi hiyo limezima jaribio la mapinduzi.

Kwa mujibu wa Jenerali Jamal Omar maofisa 12 na askari wanne wamekamatwa kuhusiana na jaribio hilo ambapo  amesema maofisa hao wanatoka jeshini na idara za usalama za nchi, baadhi yao wakiwa wamestaafu.

 

Akizungumza kupitia televisheni, amesema tukio hilo ni njama za kukwamisha makubaliano yaliyofikiwa baina ya baraza la kijeshi la mpito na muungano wa uhuru na mabadiliko.

 

Taarifa hiyo iliyotolewa usiku wa jana, inakuja wakati washauri wa kisheria wa baraza hilo na viongozi wa waandamanaji wakijadiliana juu ya makubaliano ya wiki iliyopita juu ya kugawana madaraka,  katika mazunguzo yaliyofanikishwa na Umoja wa Afrika na ujumbe wa Ethiopia.

 

Wakati huohuo, mtandao wa Intaneti umerejeshwa nchini humo kuanzia siku ya Jumatano wiki hii.

Comments are closed.