The House of Favourite Newspapers

 Sven Afunika Makocha Wote Ligi Kuu

0

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba, amekiongoza kikosi hicho kwenye jumla ya mechi 18 tu, lakini amewafunika makocha wote walioviongoza vikosi vyao tangu mwanzoni mwa msimu.

 

Sven alichukua nafasi ya Patrick Aussems tangu Desemba, mwaka jana lakini timu yake imefunga mabao mengi zaidi tangu alipoichukua, zaidi ya timu zote tangu mwanzo wa msimu.

 

Amefungwa mechi mbili na kulazimisha sare moja huku akiwa ameshinda mechi 15 za ligi kuu. Timu yake imefunga mabao 46 na kufungwa 12, ikiwa kileleni mwa msimamo kwa pointi 71 na imefunga jumla ya mabao 63.

 

Sven amekuwa na matokeo ya hatari Bongo kwani kwa idadi ya mabao ya kufunga tu, amezifunika timu zote ndani ya Ligi Kuu Bara.

 

Hata wapinzani wake wakubwa walio kwenye tano bora, ukichukua takwimu zao za tangu mwanzo wa msimu, hawafui dafu kwa Simba ya Sven ya mechi 18 tu.

Azam iliyo nafasi ya pili ikinolewa na Aristica Cioaba imefunga mabao 37, imecheza mechi 28, Yanga iliyo chini ya Luc Eymael nafasi ya tatu imefunga mabao 31, imecheza mechi 27.

 

Namungo iliyo chini ya Hitimana Thiery, nafasi ya nne imefunga mabao 34 ikiwa imecheza mechi 28, Coastal Union iliyo chini ya Juma Mgunda imefunga mabao 27 ikiwa imecheza mechi 28.

Matokeo yake katika mechi 18 yapo namna hii, sare:-Januari Mosi, Simba 2-2 Yanga. Kichapo:- Februari 7, JKT Tanzania 1-0 Simba, Machi 8, Yanga 1-0 Simba.

 

Mechi 15 za ushindi hizi hapa:-Septemba 25, Simba 4-0 Lipuli, Septemba 28, KMC 0-2 Simba, Februari 31, Simba 2-0 Ndanda, Januari 16, Mbao 1-2 Simba, Januari 19,Alliance 1-4 Simba, Januari 29,Simba 3-2 Namungo, Februari Mosi, Simba 2-0 Coastal Union.

 

Simba 2-1 Polisi Tanzania, Februari 2, Februari 11, Mtibwa Sugar 0-3 Simba, Februari 15, Lipuli 0-1 Simba, Februari 18, Simba 1-0 Kagera Sugar, Februari 22, Simba 3-1 Biashara United, Machi Mosi, Simba 2-0 KMC, Machi 4, Azam 2-3 Simba, Machi 11, Simba 8-0 Singida United.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply