SIWEZI KUZEEKA , SINA STRESS – MONALISA

Yvonne Cherry

 MUIGIZAJI wa kitambo Bongo, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ amesema kuwa hawezi kuzeeka kwa sababu hana kabisa stress na ndiyo maana kila siku anaonekana mrembo. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Monalisa alisema kuwa mara nyingi amekuwa akiulizwa swali la nini anatumia kiasi cha kumfanya asizeeke lakini anaeleza kwamba siri ya kuwa hivyo ni kutokana na muda mwingi kuwa na furaha na kutokuwa na stress za maisha.

“Mimi kwa kweli sina stress na sio kwamba sina matatizo ila niliamua sio kila jambo baya au linaloniumiza nalibebe, huwa naamua kuyapotezea kwa sababu nikisema nibebe dunia hii kuna mambo mengi, nitazeeka bure,” alisema Mona. Akasema kuwa mara, nyingi amekuwa na mbinu nyingi za kutafuta nini cha kufanya ili kichwa chake kiwaze kazi na sio kushindwa au kuwaza kitu ambacho kitamfanya akose amani.


Loading...

Toa comment