The House of Favourite Newspapers

Tabasamu Ashinda Ubunge Sengerema – Video

0
MSIMAMIZI  wa uchaguzi jimbo la Sengerema, Magesa Mafuru, leo Oktoba 29, 2020, amemtangaza mgombea ubunge wa Jimbo la Sengerema, Hamis Tabasamu Mwangao,  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo huku akiwaburuza wenzake wa upinzani.
Aidha, CCM imeshinda udiwani kata zote 26 za jimbo hilo.
Matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Sengerema
Vituo vya kupigia kura vilikuwa 157
Jumla ya wapiga kura walioandikishwa ni 200,692
Kura zilizopigwa 70,126 Kura halali 68,180
Kura zilizokataliwa 1,946.
Matokeo
Mchele John Mathias (CUF) kura 497
Victoria Benedict Batangile (Chadema) kura 7,949
Tabasamu Hamisi Mwangao (CCM) kura 59,734.

Leave A Reply