The House of Favourite Newspapers

Tajiri Aliyevamia Na Kujenga Eneo La Mjane Kukutana Na Waziri Silaa – Video

0

Mwanamke mjane, Marietha Kalonga mkazi wa jijini Mbeya, amemwaga machozi mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa wakati akimueleza jinsi alivyodhulumiwa ardhi yake na mfanyabiashara mmoja jijini Mbeya aliyejenga nyumba kwenye kiwanja chake.

Baada ya kusikiliza malalamiko hayo, Silaa amemtaka mfanyabiashara huyo kuvunja mwenyewe nyumba yake kabla ya Jumatano (keshokutwa) na kuahidi kumshughulikia kikamilifu ili haki itendeke na mjane huyo apewe ardhi yake.

Silaa na timu yake wanaendelea kusikiliza malalamiko na kero za ardhio katika Ukumbi wa Mkapa, Sokomatola jijini Mbeya.

Leave A Reply