The House of Favourite Newspapers

Tamasha Kubwa la Speakers Conference Kutimua Vumbi Jumamosi Hii

0

Tamasha kubwa la Speakers Conference, linatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, Novemba 28, 2020 katika Ukumbi wa City Mall, Mnazi Mmoja mkabala na Chuo cha DIT jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wazungumzaji mahiri kutoka ndani na nje ya nchi.

 

Kwa mujibu wa mwanzilishi na mratibu wa tamasha hilo, Rodrick Nabe ambaye pia ni Mkurugenzi wa Road to Success Initiative, tamasha hilo litaanza saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni na kwa mwaka huu, linatarajiwa kuweka historia ya aina yake kutokana na idadi kubwa ya wazungumzaji wa kimataifa (international speakers) watakaohudhuria.

 

“Viingilio vipo vya aina tatu, VVIP ni shilingi 100,000 (laki moja), VIP ni shilingi 50,000 huku kawaida ikiwa ni shilingi 30,000 na tiketi zinapatikana ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa namba 0674502925,” alisema Rodrick na kuongeza:

 

“Hili ni tamasha la tatu, la kwanza lilikuwa ni mwaka 2018 na lilifanyikia Mafao House, Dar es Salaam, baadaye likafanyika tena mwaka 2019 katika Ukumbi wa Ubungo Plaza na kuwakutanisha wazungumzaji kutoka Tanzania, Botswana na Kenya.

 

“Tofauti na matamasha yote yaliyotangulia, tamasha la mwaka huu litaweka historia ya aina yake na kila atakayehudhuria, ataondoka akiwa amepata kitu kikubwa sana kitakachoenda kuyabadili kabisa maisha yake.

 

“Tunao wazungumzaji wenye nguvu kubwa kutoka ndani ya Tanzania, wakiwemo mimi mwenyewe (Rodrick Nabe), Eric Shigongo, Anthony Luvanda, Mwalimu Makena, Faraja Nyalandu, Harris Kapiga, Lucas malembo, Alice Nchwali, Dr Chriss Mauki na Aunt Sadaka lakini kama hiyo haitoshi, kutakuwa na wazungumzaji watoto, Restiel Kilongola na Grace Owden.

 

“Pia ipo orodha ndefu ya wazungumzaji kutoka nje ni ndefu, akiwemo Nguvulu Vincent kutoka nchini Zambia na wengine wengi.

 

“Pia kutakuwa na ‘special appearance’ ya watu mbalimbali mashuhuri, kuanzia kwa motivational na insipirational speakers, wajasiriamali wadogo wkwa wakubwa, waandihi wa habari, watangazaji, watunzi wa vitabu na watu kutoka kada nyingine mbalimbali.

 

Mbali na wazungumzaji hao, lakini pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wachekeshaji (stand up commedy), ambao pia watakuwepo siku hiyo kuhakikisha watu wote wanajifunza mambo makubwa maishani mwao lakini wakati huohuo wakipata burudani nzuri.

 

HISTORIA YA JINSI TAMASHA LILIVYOANZA

Akizungumza na Ijumaa, mratibu wa tamasha hilo, Rodrick anasema alipata wazo la kufanya kongamano ambalo lingewakutanisha wazungumzaji kutoka ndani na nje ya nchi lakini hakuwa anajua ni wapi ataanzia.

 

“Nilikuwa na hofu kubwa sana kwenye moyo wangu kwa sababu bado nilikuwa mchanga kwenye tasnia ya public speaking. Nikamshirikisha rafiki yangu wa karibu, Rev. Ipyana Mwakamela ambaye aliniambia kwamba kitendo cha mimi kupata wazo la kufanya kongamano hilo, ilikuwa ni sauti ya Mungu, akanitia moyo na kuniambia kwamba uwezekano wa kufanikisha ndoto zangu ni mkubwa,” anasema Rodrick.

 

Baada ya hapo, alifunga safari mpaka jijini Nairobi, Kenya ambako alikutana na wazungumzaji wawili wakubwa, Alfred Ogola na Radido Dooso ambao walimpa ushauri wa njia za kupita ili hatimaye afanikishe tukio hilo.

 

“Tulikunywa kahawa pamoja, wakanipa mbinu ambazo ziliamsha ari kubwa ndani ya moyo wangu, nikaondka Nairobi kurudi Dar es Salaam nikiwa na munkari wa kutosha. Nikakutana na mentor wangu na kumueleza nilichojifunza Nairobi na bila kupoteza muda, utekelezaji ulianza.

 

“Tulihakikisha kila kitu kinaenda vizuri, mipango yote ikakaa sawa, matangazo yakaanza kurushwa kwenye vyombo vya habari na hatimaye msimu wa kwanza wa Speakers Conference ukafanyika Septemba, 2018 katika ukumbi wa Mafao House, Dar es Salaam.

 

Rodrick anaendelea kueleza kwamba mwaka uliofuatia, tamasha hilo pia lilifanyika kwa mafanikio makubwa ambapo washiriki zaidi ya 500 wakajifunza kuhusu sanaa ya kuzungumza mbele ya kadamnasi, ujasiriamali na maendeleo binafsi.

 

“Mwaka huu, 2020 ni awamu ya tatu. Lengo letu kubwa ni kuiinua tasnia ya ‘publick spkeaking na kuitengenezea thamani. Ninachoamini ni kwamba hata kama itachukua miaka mingi, ipo siku atafikia malengo yake kwa sababu mafanikio ni mchakato.

 

“Viingilio vipo vya aina tatu, VVIP ni shilingi 100,000 (laki moja), VIP ni shilingi 50,000 huku kawaida ikiwa ni shilingi 30,000 na tiketi zinapatikana ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa namba 0674502925,” alihitimisha Rodrick.

Na Mwandishi Wetu

Leave A Reply