The House of Favourite Newspapers

Tamasha la Bodaboda Kutikisa Dar, Trafiki na Waendesha Bodaboda Kusakata Soka

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JP Decaus, Elia Richard akizungumza na wanahabari.

TAMASHA la Pikipiki maarufu kama Tamasha la Bodaboda linatarajia kutikisa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JP Decaus ambao ni waratibu wa  tamasha hilo, Elia Richard alisema kuwa wameandaa tamasha hilo kwa wadau wa sekta ya bodaboda linaloitwa ‘Dar Bodaboda Superstar Unity Festival’ ambalo litafanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji, Shaban Makugaya (katikati) akizungumza na wanahabari.

Alisema kuwa JP DECAUS ni Kampuni inayojishughulisha  na kazi za mawasiliano, mahusiano na matangazo  sambamba na uandaaji wa mikutano. “Bodaboda superstar ni onesho linalojumuisha burudani,Elimu ambalo limetenga kuwaleta Pamoja  watu wote na sekta ya bodaboda Nchini”

Aidha Siku hiyo elimu mbalimbali juu ya uendeshaji ulio salama na kuzingatia Sheria za barabarani utatolewa.

Pia kutakuwa na mechi kati ya timu ya trafiki na waendesha bodaboda huku burudani kutoka kwa wanamuziki wa kizazi kipya, taarabu na singeli watakuwepo ili kunogesha tamasha hilo.  

                      

Naye Mkurugenzi Mtendaji, Shaban Makugaya akizungumzai tamasha hilo alisema tamasha hilo litafanyika Mei 13 mwaka huu na kutakuwa likifanyika kila mwaka nchi nzima ambapo jina la maonesho hayo litakuwa likibadilika kulingana na mji au mkoa litakaokuwa limefanyika.

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply