The House of Favourite Newspapers

Tamasha la Campus Tour Latingisha Jijini Mbeya, Wasanii Kibao Watumbuiza

0

Tamasha kubwa la muziki la Campus Tour limetingisha katika Viwanja vya Chuo cha Uhasibu jijini Mbeya, ambapo wasanii kibao wametumbuiza.

Tamasha hilo limewajumuisha wanafunzi wa vyuo vikuu vinne jijini Mbeya ikiwemo Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), limeandaliwa na jukwaa la muziki la Boomplay na wadau wengine.

Tamasha hilo limehitimisha ziara ya wiki nne ya kiburudani, iliyodhaminiwa na platform ya kusikiliza muziki ya Boomplay kwa kushirikiana na simu ya kijanja ya TECNO Camon 20 Series na kinywaji cha Desperados ambayo ililenga kusherehekea ubia mzuri wa muziki na teknolojia na kuacha alama isiyofutika jijini humo.

Kampeni hiyo ilishuhudia nguvu ya ushirikiano, ikiwaleta pamoja vinara wawili wa tasnia ili kuzungumza na kuburudisha jumuiya ya wanafunzi wanaopenda masuala ya burudani.


Katika muda wote wa ziara hiyo, wanafunzi waliweza kushirikishwa kwenye shughuli mbalimbali sambamba na burudani ya muziki.

Kuanzia kwemye shoo ya muziki kutoka kwa wasanii maarufu wa hapa nchini hadi maonyesho ya teknolojia shirikishi yanayoonyesha ubunifu wa hali ya juu zaidi wa TECNO, tukio lilitoa hali nzuri ambayo ilichanganya muziki na teknolojia kikamilifu.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli alieleza kufurahishwa kwake na mafanikio makubwa ya Kampeni hiyo akisema, “Mwaka huu tunafuraha kubwa kushirikiana na TECNO na Desperados kwa tukio hili la kipekee.

 

“Muziki una uwezo wa kuvuka mipaka na kuleta watu pamoja, na ushirikiano wetu umedhihirisha hilo,” alisema.

Akizungumzia Kampeni hiyo, Mkuu wa kitengo cha Masoko wa TECNO Tanzania, Salma Shafii alisema:

“TECNO, tunaamini katika kutumia teknolojia ili kuongeza uzoefu wa watumiaji wetu kwa jumla.”

Leave A Reply