The House of Favourite Newspapers

Tamasha La Pasaka Hakuna Kiingilio, Ni Bure Bila Kiingilio – Msama

0
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (kulia) akitangaza tamasha hilo mbele ya wanahabari.

Tamasha kubwa la Pasaka linanatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Leader’s Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar, Aprili 9 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion ambaye pia ni Mwandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama amesema tamasha hilo litakuwa la tofauti na matamasha mengine yaliyowahi kupita.

Msama amesema katika tamasha hilo waimbaji wote wataimba kwa kupigiwa vyombo mubashara ili kuongeza radha ya burudani na kubwa zaidi hakuna kiingilio.

Kuhusu usalama Msama alisema katika tamasha hilo kutakuwa na usalama wa hali ya juu kwa watu na mali zao na kuwaomba wananchi kuja kufurika kwenye tamasha hilo ili wajionee burudani hiyo itakayoacha gumzo.

“Katika kipindi hiki cha Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan tumeona mambo mengi yanaenda vizuri sana hivyo nasi tumeamua kuandaa tamasha hili kubwa na la aina yake ndio maana kutakuwa na wasanii wakubwa ambao wanafanya vizuri katika muziki wa injili. “Kuna wasanii wengi wakubwa wa muziki wa injili kutoka nje ambao wengine hawajawahi kufika hapa nchini nao watakuja kupiga shoo hiyo hapa nchini kwa mara yao ya kwanza. Msama alimaliza kusema.

Leave A Reply