The House of Favourite Newspapers

Tambwe Abeza Kambi Ya Kimba Uturuki

AMISSI Tambwe ambaye msimu uliopita hakufanya lolote ndani ya Yanga, amedai kwamba hatishwi na kambi ya Simba huko Uturuki wala uzoefu wa mastaa waliowasajili.

 

Tambwe ambaye habari zinadai amenusurika kutemwa na Yanga kutokana na hali mbaya ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo amesema kwamba; “Kwa upande wetu wasitarajie mteremko maana mechi ambazo tunacheza sasa zinatujenga kwa kuirudisha miili yetu kwenye wakati wake kabla ya kuanza ligi.”

 

“Tunajua tunacheza nao lini labda wao wanaweza pengine kujivunia wachezaji ambao wamewasajili lakini hata Yanga imesajili kwa ajili ya michuano yote kikubwa kwao wao na wajue tunafanya maandalizi ya kucheza na timu zote bila kujali walikuwa wapi katika maandalizi yao ya msimu kwa sababu tunajipanga kurejea kwenye nafasi yetu,” alisema Tambwe ambaye ni raia wa Burundi.

Comments are closed.