The House of Favourite Newspapers

Tambwe Kaanza Kiburi Akiwa Benchi

0
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe.

STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe amesema hali yake kwa sasa siyo mbaya sana na muda wowote atarudi uwanjani, lakini amepiga mkwara kwa kusema anataka kufukuzana kwa ufungaji na mfungaji bora.

 

Emmanuel Okwi wa Simba ndiye anayeongoza kwenye orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao nane, sasa Tambwe anasema akirudi uwanjani atahakikisha anamfikia.

Tambwe amedai anatamani sana Okwi asiongeze bao lolote katika kipindi hiki mpaka yeye atakapoanza kuitumikia Yanga.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe alisema anaamini akirudi uwanjani na asipopata majeraha tena basi ndani ya mechi tatu au nne anaweza kufikisha mabao nane yaliyofungwa na Okwi.

 

“Hali yangu kwa sasa siyo mbaya sana ninamshukuru Mungu naendelea vizuri lakini pia naomba ligi isimame kwa muda hata mechi yetu ijayo na Mbeya City natamani isiwepo ili niweze kupona vizuri.

 

“Nataka siku nikirudi niweze kuwa fiti zaidi tayari kwa kupambana na akina Okwi na wenzake ambao hivi sasa wanachuana kwa kuzifumania nyavu,” alisema Tambwe.

 

Tambwe anayesumbuliwa na goti bado hajaanza mazoezi lakini mwenyewe amedai ndani ya siku chache zijazo atarejea uwanjani huku akijitibu binafsi.

Leave A Reply