The House of Favourite Newspapers

Tambwe Kumwaga Machozi

0

MSHAMBULIAJI wa DTB, Amissi Tambwe amesema kuwa changamoto kubwa ambayo wanakumbana nayo katika ligi daraja la kwanza ni kuchezewa mpira wa kihuni kutokana na ligi hiyo kutoonyeshwa kwenye televisheni.

Tambwe mpaka sasa amefanikiwa kuifungia DTB mabao sita katika michezo minne aliyocheza katika ligi daraja la kwanza.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Tambwe alisema kuwa kwenye ligi daraja la kwanza mabeki wa ligi hiyo wamekuwa wakicheza mpira wa kihuni kwa kuwa wanafahamu kuwa hawaonekani popote tofauti na ligi kuu jambo ambalo linawaumiza sana washambuliaji wa ligi hiyo.

“Ligi daraja la kwanza kuna uhuni sana unafanyika haswa kwa mabeki wengi hucheza soka la ajabu huku wakiamini kuwa hawaonekeni sehemu yeyote kwa kuwa ligi hiyo haionyeshwi kwenye televisheni.

“Kwenye ligi kuu ni ngumu mabeki wengi kucheza mpira wa kihuni kwa kuwa wanafahamu kuwa wanaonekana na ligi inaonyeshwa kwenye televisheni tofauti na ligi daraja la kwanza, kwa kweli washambuliaji tunaumizwa sana,”alisema Tambwe.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave A Reply