The House of Favourite Newspapers

Tambwe Siyo Nguzo Yanga, Juhudi za Pamoja Zinahitajika

0
Amissi Tambwe

UNAPOTHUBUTU kuzungumzia wachezaji wazuri katika safu ya ushambuliaji kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huwezi kuliacha hata kwa bahati mbaya jina la Amissi Tambwe anayechezea Yanga.

 

Kijana huyu raia kutoka nchini Burundi amejizolea sifa nyingi na kufanikiwa kuliweka jina lake kwenye ramani ya soka siyo hapa nyumbani pekee bali hata nchini kwake, kutokana na umahiri wake wa kulijua goli lilipo awapo uwanjani.

 

Tambwe amekuwa mshambuliaji tegemeo kwenye klabu yake ya Yanga na kusaidia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio iliyonayo mpaka wakati huu, jambo linalosababisha kuaminika sana na wakuu kunako benchi la ufundi.

 

Amekuwa pia msaada mkubwa kwenye timu yake ya Taifa ya Burundi kiasi cha kuitwa mara kwa mara kunapokuwepo na mashindano mbalimbali yanayolihusisha taifa lake licha ya kwamba hana mafanikio makubwa kwenye kikosi hicho cha Intamba Murugamba. Tangu kuanza kwa msimu huu 2017/18 wa ligi kuu, nyota huyu amekuwa akisumbuliwa na majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu akiiacha klabu yake
ikipambana kusaka pointi muhimu ili kujisafishia njia ya kuutetea tena ubingwa kwa urahisi.

 

Pengine ni jambo la faraja mno kwa wanachama na mashabiki wa Yanga kuona Tambwe amerejea tena mzigoni baada ya kimya cha muda mrefu akiwa majeruhi, w e n g i wao waki s e m a ; “Afadhali mtambo wa magoli umerudi kazini.” Hii ni hali ya kawaida kwa mashabiki kuwa na mategem e o makubwa juu ya mchezaji fulani, lakini ukweli utabaki palepale kwamba hata awe na kiwango kizuri kupitiliza kama hapati ushirikiano na juhudi za wachezaji wenzake uwanjani ni vigumu kufurukuta. Kwa mechi tano ilizocheza Yanga mpaka sasa imefanikiwa kuvuna na kuweka kibindoni alama tisa baada ya kupata ushindi katika mechi mbili na kupata sare kwenye mechi tatu wakiwa na jumla ya mabao manne, matokeo ambayo hayajawafurahisha mashabiki kutokana na ushindani mkali uliopo kwenye ligi msimu huu.

 

Kurejea kwa Tambwe pekee hakutoshi kubadili hali hiyo ya ufinyu wa upatikanaji wa mabao mengi bila ya kuwepo na juhudi za kujituma kwa nguvu kutoka kwa wachezaji wenzake ambao nao wana jukumu la kuipigania klabu yao. Wapo mashabiki wanaolalamika kwamba hawafurahishwi na kiwango kinachoonyeshwa na timu yao tangu ligi ilipoanza, wengine wakienda mbali zaidi kwa kuthubutu kuwataja kwa majina wachezaji wanaocheza kwa kuzembea na kwa dharau kubwa dhidi ya wapinzani wao.

 

Kama hivyo ndivyo, basi Kocha Mkuu George Lwandamina anapaswa kubadili mtazamo kwa vijana wake wanaoonekana kutaka kumuangushia jumba bovu, kwa kuongeza ukali kwenye mazoezi na ikiwezekana kuwapangia malengo maalum kila mmoja wao na asiyetimiza ampokonye namba na kupewa mwingine. Mfumo huu ndiyo unaotumika kwenye klabu nyingi duniani tena ambazo zimeendelea sana kisoka kiasi cha kuwafanya wachezaji kujituma zaidi kulinda nafasi zao.

Ngoma na Chirwa Kuondoka Kikosini Kisa Hiki Hapa

Leave A Reply