The House of Favourite Newspapers

Tammy: Amkumbuka Ngwea kwa The Baddest

0

tammy (1)Na Andrew Carlos

STAA wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Tamara Ally ‘Tammy The Baddest’ amefungukia kati ya vitu ambavyo hatavisahau maishani ni pamoja na kupewa jina la The Baddest na marehemu Albert Mangweha ‘Ngwear’.

Akizungumza na Showbiz, Tammy anayebamba na Ngoma ya Trumpet alisema kuwa Ngwear alikuwa kama kaka yake aliyekuwa akimsaidia mambo mengi kimuziki.

“Alipenda kuniita The Baddest na kunihimiza nisikate tamaa ya kutoka, kikubwa niendelee kuandika, kurekodi na kusambaza. Leo hii namuenzi kwa kuendelea kutumia jina la The Baddest,” alisema Tammy anayetambulika pia kama Nicki Minaj wa Bongo.

Leave A Reply