The House of Favourite Newspapers

Tanasha Awalipua Kimtindo Zari, Mobeto

0

 

AMERUSHA mawe gizani! Si mwingine bali ni mrembo kutoka Kenya, Tanasha Donna Oketch ambaye ni mpenzi wa msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Tanasha ambaye pia ni mzazi mwenza wa Diamond, amerusha mawe hayo kwa kuandika waraka kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwalenga wapenzi wa zamani wa Diamond yaani Zarina Hassan ‘Zari’ na Hamisa Mobeto.

 

Licha ya kwamba Tanasha hakutaja majina, lakini wafuasi kwenye ukurasa wa mwanadada huyo walihitimisha kuwa waraka wake ulikuwa ukiwalenga wapenzi wa zamani wa Diamond au Mondi.

 

Tanasha ambaye pia ni mtangazaji katika kituo cha redio cha NRG nchini Kenya, aliwahimiza walengwa wake kuishi kwa maisha yao halisi badala ya kuishi maisha feki na kurusha picha mitandaoni kwa lengo la kuwahadaa wapenzi wao wa zamani.

 

Katika ukurasa wake wa Instagram wa Tanasha ambao Risasi Jumamosi limeusoma Disemba 18 mwaka huu, Tanasha alirusha mawe hayo gizani ambapo aliandika waraka mrefu akihimiza walengwa wake kutoishi maisha feki kwa lengo la kuwafanya wapenzi wao wa zamani waone wivu.

 

‘’Maneno ya busara Jumatano; Kamwe usilazimishe kile ambacho hakina maana yoyote kwako, kama Ex wako wa kiume au wa kike havutiwi chochote kutoka kwako, hawezi kuwa mpenzi wako tena.

 

“Kutuma picha mpya, na kuosha mjini kwa magari na fasheni mbalimbali ili kumvutia, ni sawa na kutumia kivuli chako ili kuingia kwenye moyo wake, au kupiga picha na mwanaume, mwanamke mwingine ili kumfanya ex wako kupata wivu dhidi yako, ni jambo ambalo haliwezi kutokea, unapoteza muda bure,” aliandika Tanasha.

 

Maneno hayo yaliashiria ukweli kuwa malengo ya Hamisa na Zari yalikuwa ni kuwa pamoja na Diamond lakini sasa malengo hayo yamepotea, hivyo wanapaswa kuruhusu hali hiyo.

 

‘’Fanya kinachokufaa. Zingatia unachofanya kwa maendeleo yako. Iwapo kama anataka kuwa na wewe kimapenzi, atafanya hivyo. Sio lazima ufanye mambo haya yote kuwafanya wakutambue au na watambue sababu ya anguko la mapenzi yenu. Suala la muhimu jipende, na jipange mwenyewe,” aliongeza.

 

Wakati mtangazaji huyo wa redio akitiririka bila kutaja majina, baadhi ya wafuasi wake kwenye mtandao huo walihitimisha kuwa ni wapenzi wa zamani wa Diamondi, yaani Zari na Hamisa.

 

Chapisho hilo la Tanasha lilikuja siku chache baada ya Hamisa kupakia kwenye mitandao ya kijamii picha zenye maelezo kuwa kajinunulia gari kama ishara ya zawadi kwenye siku yake ya kuzaliwa.

 

Wengi waliomuunga mkono walidai kuwa alikuwa akijaribu sana kupambana na wapenzi wa zamani wa Diamond.

Zari kwa upande mwingine amekuwa busy kuuaminisha ulimwengu jinsi mpenzi wake wa sasa maarufu kama ‘King Bae’ alivyo na mapenzi motomoto kwa mwanamama huyo mwenye asili ya Uganda.

Stori: MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply