The House of Favourite Newspapers

Tanga: Ajali Mbaya Yaua Sita Papo Hapo

WATU watano wamefariki dunia papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya, baada ya basi kubwa kugongana na Hiace katika eneo la Kabuku wilayani Handeni.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Leonce Rwegasira alisema ajali hiyo ilitoke saa 5:30 asubuhi katika eneo hilo la Kabuku.

Alitaja magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi la Kampuni ya AJ Safari lililokuwa likitoka Lushoto kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Khalifa Mussa Omary mkazi wa Chamanzi Dar es Salaam lenye namba za usajili T 497 BJB mbalo limegongana na Hiace iliyokuwa ikitoka Mkata kwenda Segera yenye namba T591 AKE.


Aliwataja waliokufa kuwa ni pamoja na dereva wa Hiace aliyefahamika kwa jina moja la Shabaan, wengine majina yao hayajatambulika na maiti zao zimehifadhiwa Kwenye Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.

ACP Rwegasira alisema majeruhi ambao hawakuchukuliwa majina yao kutokana na uharaka wa kuwasaidia kuwafikisha katika Kituo cha Afya Kabuku kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

IGP Sirro Alivyomuapisha Kamishina wa Polisi Zanzibar Leo!

Comments are closed.