The House of Favourite Newspapers

Tanzania Kuwa Mwenyeji wa Jukwaa la Mtandao wa Chakula Afrika

0

 

Rais Samia Suluhu Hassan, ameridhia Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kilimo utakaohusisha viongozi, watu mashuhuri na wadau wapya wapatao 3,000.

 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa uamuzi huo umetangazwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn katika Jukwaa la Mtandao wa Chakula Afrika (AGRF) lililofanyika nchini Marekani.

 

 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Rais Samia amesema anatarajia mkutano huo utaendeleza uimarishaji wa mifumo ya chakula na kilimo katika vipaumbele vya serikali, kupeana taarifa na kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya mifumo imara ya chakula.

 

Leave A Reply