The House of Favourite Newspapers

Tanzania Kuzitoza Kodi Facebook, Twitter, Instagram & Apple

0

SERIKALI ya Tanzania imesema inatarajia kuanza kuyatoza kodi makampuni ya Google, Facebook, Instagram, Twitter, Apple na yote yanayoendesha huduma za mitandao ya kijamii nchini.

 

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia ukurasa wake wa Instagram amendika kuwa wanafikiria kuanza kuwatoza kodi wamiliki wa makampuni hayo ya kigeni kwa sababu yanapata fedha na hayalipi kodi. Hata hivyo, Mwigulu amefafanua kuwa kodi hiyo haiwahusu watumiaji bali wamiliki wa makampuni hayo.

 

Ujumbe wa Mwigulu

Tunategemea (tunatafuta namna) kuwatoza kodi kama nchi zingine zinavyofanya kwa wamiliki wa Google, Twitter, Facebook, Instagram, Apple na Makampuni mengine kwasababu haya ni Makampuni ya Kimataifa na yanapata fedha kwa Watu wetu na hayalipi kodi. Kodi za Mitandao hazihusishi watumiaji (wananchi wanaotumia mitandao hiyo), hivyo watu wasipotoshe.

Serikali imesema imeanza kuliangalia eneo jipya la kukusanya mapato na kwamba inakusudia kuanzisha tozo mpya ya huduma za kidigitali (Digital Service Tax) ili kupanua wigo wa makusanyo.
Mwigulu amewaambia waandishi wa habari Jijini Dodoma kwamba kuna huduma nyingi za kidigitali ambazo watoa huduma wanajipatia mapato bila kulipa kodi.
“Tutaziangalia hizo mnajua na mnazo kwenye simu zenu… wenyewe wanatengeneza pesa nadhani bado mapema kuzisema,” alisema wakati akitolea ufafanuzi marekebisho ya tozo ya miamala ambayo serikali imesema imepunguza kwa asilimia 30.
Digital Service Tax ama (DST) ni ushuru unaowekwa kwa kampuni za kimataifa kulingana na shughuli zao za kidijitali katika eneo fulani.
Mfano Uingereza, ilianzisha DST mwezi April 2020 kwa kutoza asilimia 2 kwa mapato yote yanayotokana na biashara kubwa zinazotolewa na mitandao ya kijamii. Nchi nyingine kwa Ulaya ni Italia, Austria, Spain, na Ufaransa.

Leave A Reply