The House of Favourite Newspapers

Mwakinyo: Kupigana na Kiduku ni Kama Kumuona Mtume

0

Bondia wa Kimataifa kutoka Tanga, Hassan Mwakinyo amesema uwezekano wa yeye kupigana na hasimu wake, Twaha Kiduku ni vigumu kutokea kwani Kiduku hajafikia rekodi zake na bado hajawa kwenye rank ya juu ya mabondia wakubwa duniani.

 

“Duniani kote sijawahi kusikia mabondia wanashindania magari, huwa wanapewa mikanda yenye thamani na pesa ndefu ambazo zitawafanya wanunue magari wanayotaka au waka-invest kwenye viwanda vya magari baada ya pambano. Mapromota wa Tanzania waupe thamani mchezo huu wa boxing.

 

“Kauli yangu kuwa Tanzania hakuna bondia wa kupigana nami, sio dharau, mimi nahitaji kupigana na bondia ambaye ana rekodi kama zangu au amenizidi ili nikimshinda linisogeze mbele.

 

“Kwa sasa Pambano langu na Twaha Kiduku haliwezi kutokea kama ambavyo ilivyo ngumu kumuona Mtume. Halipo na sipigani kuwafurahisha watu hii ni biashara yangu. Ukitaka kupigana na mimi tafuta rekodi zako ufike nilipo labda tunaweza kujadiliana na sio kulazimishana,” amesema Mwakinyo.

Leave A Reply