The House of Favourite Newspapers

Tanzania U-23 Yafuzu Nusu Fainali Cecafa

0

Timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 (U-23) imefuzu kwa hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda katika michuano hiyo ya Afrika Mashari na Kati (CECAFA).

 

Katika mechi hiyo iliyomalizika muda mfupi uliopita ambapo mwenyeji wa mashindano hayo ni Ethiopia, mchezaji Lusajo ndiye aliyepachika bao kwa Tanzania kabla ya Uganda kusawazisha.

 

Tanzania imefuzu hatua hiyo baada ya kushinda mchezo mmoja na sare moja kuwa na jumla ya pointi nne.

Leave A Reply