The House of Favourite Newspapers

Tanzania, Uganda Kujenga Umeme wa Maji Kikagati-Murongo

SERIKALI za Tanzania na Uganda zinatekeleza ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Kikagati-Murongo, uliopo kwenye mto Kagera mpakani mwa nchi hizo mbili utakaozalisha megawati 14. Inakadiriwa kuwa kila nchi itapata megawati saba kati ya hizo baada ya  kukamilika.
Mradi huo unajengwa na kampuni ya PAC ya Italia na unasimamiwa na kampuni binafsi ya Uganda ya Kikagati-Murongo Hydropower Project ambayo ndiyo mjenzi wa mradi huo ulioanza Mwezi Mei 2018 na kutarajiwa kukamilika Mei 2021 kwa gharama ya Dola Milioni 90.
Mradi huo ni makubaliano ya nchi hizo mbili  kuhusu matumizi bora ya maji ya mto Kagera ambao upo mpakani mwa nchi hizo.
Geoffrey Mwambe aliyetembelea eneo la ujenzi huo  ametaka maazimio ya asilimia 50 kila upande wa nchi hizo mbili  yazingatiwe.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Generali Marco Gaguti, amesema kukamilika kwake kutasaidia kupatikana kwa umeme wa uhakika mkoani kwake.
Naye Mhandisi Mshauri wa Mradi huo kutoka Kampuni ya  Nishati ya Geni, Mhandisi Dkt Juliana Pallangyo,  alisema watasimamia ipasavyo kufanikisha ujenzi huo kuwa kila nchi itanufaika.
Mradi huo unajengwa wilayani Kyerwa, mkoani Kagera  kwa Tanzania na Wilaya ya Isingilo, Uganda

Comments are closed.