The House of Favourite Newspapers

TANZIA: ASKOFU CHENGULA AFARIKI DUNIA

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya, Evaristo Malcus Chengula (pichani) amefariki dunia asubuhi ya leo (Novemba 21, 2018) wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TEC, Padri Charles Kitima, Askofu Chengula alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa moyo yaliyochangiwa na umri wake ambapo amefariki akiwa na miaka 78.

“Baba Askofu hakuwa anaumwa sana lakini alikuwa na tatizo la Moyo ambalo alikuwa analimudu kawaida na alikuwa anaendelea na kazi kama kawaida mpaka Alhamisi iliyopita ameongoza misa takatifu hali ilipobadilika ndipo alimtafta daktari wake”, amesema Padre. Kitima.
Padre Kitima amesema kuwa Askofu Chengula atazikwa jijini Mbeya siku ya Jumanne katika kanisa alilokuwa akihudumia Askofu.

Askofu Chengula alizaliwa Januari Mosi, 1941 na amedumu katika huduma ya upadre katika Shirika la Consolata hadi mwaka 1997 alipoteuliwa kuwa Askofu.

SIMANZI! AJINYONGA KIKATILI UKIKIJUA KISA UTASHANGAA!

Comments are closed.