The House of Favourite Newspapers

TANZIA: Baba Mzazi wa Amina Chifupa Afariki Dunia

0
Mzee Hamiss Chifupa enzi za uhai wake.

TANZIA: Baba mzazi wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum, marehemu Amina Chifupa, Mzee Hamiss Chifupa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwa mwanaye wa kike, Upanga, jijini Dar es Salaam.

 

Mjuu wa Marehemu ambaye pia ni mtoto wa Marehemu Amina Chifupa, Abdulrahman Mpakanjia.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya mzee Chifupa zinasema mzee huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kiharusi lililompata toka wiki iliyopita, ambapo alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kutolewa mapema wiki hii baada ya kupata nafuu.

Mdogo wa Marehemu Mzee Chifupa, Rajab Issa akielezea namna ambavyo msiba wa kaka yake umewakumba.

“Baada ya kumtoa Muhimbili tulimpeleka kwa mwanaye wa kike Upanga na jana majira ya jioni alianza kulalamika kuwa hapumui vizuri na majira ya saa mbili za usiku tukiwa katika harakati za kumpeleka hospitali alifariki dunia,” alisema Rashid Issa mdogo wa marehemu na kuongeza kuwa;

Nyumbani kwa marehemu.

“Taratibu za mazishi bado zinaendelea hapa nyumbani kwake Mikocheni ‘B’ na tamko kuwa tutazika lini litatoka baada ya watoto wake waliyopo nje ya Dar es Salaam kufika msibani.”

Amina Chifupa na aliyekuwa mumewe, Mohammed Mpakanjia enzi za uhai wao.

Baba Mzazi wa Amina Chifupa Afariki Dunia, Mtoto wa Amina Anena

Leave A Reply