The House of Favourite Newspapers

TANZIA: Mfanyakazi wa Global Afiwa na Mama’ke

0

Heladius Banzi (kushoto mwenye shati ya drafti) akibeba jeneza lenye mwili wa mama yake  tutoa nje.
Ibaada ya mazishi ikiendelea nyumbani wkwa marehemu.
Baadhi ya vitukuu wa marehemu.
Mtoto wa kike wa marehemu akiaga mwili wa mama’ke kwa simanzi. 

 

Vilio vikitawaka wakati ndugu wakiaga.

 

Mwili wa marehemu ukiwasili kwenye makaburi ya Kigurunyembe kwa ajili ya mazishi.

Na Dustan Shekidele, Morogoro

Dereva wa Kampuni ya Global Publishers, Heladius Banzi amepata pigo baada ya kufiwa na mama yake mzazi, Antonia John aliyefariki ghafla Mei 15, mwaka huu nyumbani kwake, Kigurunyembe, Mzambarauni mjini hapa.

Mama Banzi alifariki ghafla usingizini akiwa na umri wa miaka 89. Marehemu alijaliwa kuwa na watoto 13 ambapo watano kati yao walishatangulia mbele ya haki hivyo ameacha watoto 8, wajukuu 42 na vitukuu.

Mazishi ya mama Banzi yalifanyika jana Jumatano, Mei 17, 2017 katika Makaburi ya Kigurunyembe, jirani na Chuo cha Ualimu cha Kigurunyembe mjini hapa.

PICHA: DUSTAN SHEKIDELE/GPL

Leave A Reply