The House of Favourite Newspapers

Meya wa Arusha, Waandishi 10, Wakamatwa Wakiwa Lucky Vincent

0

Wamiliki wa Shule Binafsi waliyokwenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent kufuatia ajali iliyouwa watu 35 hivi karibuni, wakiwa na waandishi wa habari wamekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.

Taarifa zimeeleza kuwa, baada ya kupata taarifa za kuwepo mkusanyiko huo, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha alifika shuleni hapo na kuwaweka ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.

UPDATES

Jeshi la Polisi limesema, Mkuu wa Mkoa Gambo ndiye aliyeamuru kuwakamata walioenda kutoa rambirambi Shule ya Lucky Vincent.

Hata hivyo Waandishi hao 10 wameachiwa huru baada ya Polisi kuwaambia waliwapa lift tu.

Eneo la Ajali ya Wanafunzi wa Lucky Vincent, Karatu

Leave A Reply