The House of Favourite Newspapers

TANZIA: MTANGAZAJI SAMADU HASSAN WA STAR TV AFARIKI DUNIA

MTANGAZAJI maarufu wa Habari wa Kituo cha Runinga cha Star Tv na Radio Free Africa, (Sahara Media Group) ambaye pia alikuwa mkongwe kwenye tasnia hiyo, Samadu Hassan amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake eneo la Miembe Mitatu, jirani na kituo cha Chakechake wilayani Nyamagana jijini Mwanza .

 

Mdogo wa Samadu, Latifa Hassan amesema kaka yake alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa zaidi ya wiki moja, kabla ya kufikwa na umauti.

 

“Jana jioni, Samadu alirudi nyumbani kwake akitokea kazini alikuwa mzima wa afya, lakini alikuwa akidai kifua kinamsumbua. Tulikula naye pamoja chakula cha jioni, akadai kifua kinamsumbua, tulimwambia twende hospitali ili akatibiwe, lakini alisema atakwenda kesho (leo).”

 

“Ilipofika saa sita kasoro usiku, ghafla hali yake ikabadilika na kuanguka chini na kuanza kutokwa na mapovu mdomoni. Tulikimbia kwenda kutafuta gari kumuwahisha hospitali, hadi tunapata gari na kurudi ndani, tulikuta tayari ameshaaga dunia,” amesema Latifa.

A to Z Mazishi ya Isaac Gamba Nyumbani Kwao Bunda

Comments are closed.