The House of Favourite Newspapers

TANZIA: MWANZILISHI WA ULINZI NA USALAMA SECURITY AFARIKI DUNIA

Mwanzilishi wa group linalojulikana kwa jina ULINZI NA USALAMA SECURITY, Yona Fares amefariki dunia jana Jumapili.

Yona alikuwa maarufu mitandaoni ambapo kifo chake kimeshtua wengi na kuacha maswali miongoni mwa watu wake wa karibu waliomfahamu.

Ujumbe alioandika kabla ya kifo chake.

“Nimekuwa kwenye matatizo ya ndoa kwa miaka 4, kila wiki nikipambana na mke mlevi na mzinzi.

“Tukio la jana usiku na leo asubuhi limenisononesha na kunitia simanzi kubwa. Nimekata tamaa ya kila kitu na kila jambo nangoja mapenzi ya Mungu tu. Nalazimika kutumia dawa za usingizi lakini wapi. Sasa nipumzike nimwache mke wangu Eng Mloelya na mchepuko wake Eng Lossy wa Idara ya Maji Mbeya waendee!”

 

“Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe.”

Comments are closed.