Tanzia: Mwenyekiti TCU Afariki Dunia

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu tanzania (TCU), Prof Mayunga Nkunya, amefariki dunia leo Jumanne, Julai 20, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu.

 

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha uhusiano na elimu kwa umma cha tume hiyo, inaeleza kuwa Katibu Mtendaji wa TCU, Prof Charles Kihampa, anatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo na kwamba tume hiyo itaendelea kukumbuka mchango wa Profesa Nkunya uliowezesha kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya TCU.


Toa comment