The House of Favourite Newspapers

TANZIA: NGULI WA MUZIKI AFRIKA, OLIVER MTUKUDZI AFARIKI DUNIA

MKONGWE wa muziki wa Jazz Barani Afrika, Oliver Mtukudzi (66) ‘Tuku’ amefariki dunia katika Hospitali ya Avenues Clinic, Jijini Harare nchini Zimbabwe leo Jumatano, Januari 23, 2019, jioni baada ya kuugua kwa zaidi ya mwezi mzima sasa.

 

Imeelezwa kuwa familia ya Mutukudzi inajipanga kutoa taarifa rasmi kuhusu kifo hicho, lakini vyombo vyote vya habri ikiwemo NewsDay na Health Times na mitandao ya kijamii nchini Zimbabwe imeripoti kifo hicho.

 

Mutukudzi ambaye alikuwa mbioni kuachia albamuyake ya 67 (Hanya’Ga), atakumbukwa kwa vibao vyake vingi vilivyotikisa Ulimwengu wa muziki, hasa wimbo wa ‘Neria’.

Oliver Mtukudzi (alizaliwa mnamo 22 Septemba 1952 mjini Highfield, Harare)  na ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu sana katika nchi hiyo ya Zimbabwe. Na alianza shughuli za muziki kunako miaka ya 1977 pale alipojiunga na bendi ya Wagon Wheels, ambayo pia alikuwemo na mwanamuziki wa zamani Bw. Thomas Mapfumo.

 

Nyimbo ya kwanza ilikuwa “Dzandimomotera” iliyoheshimika sana, na hapo ndipo Tuku alipotoa albamu yake ya kwanza, nayo pia ilileta mafanikio makubwa kabisa. Mtukudzi nae pia ni mmoja wa wanakundi la Mahube, kundi la muziki la nchi za Afrika ya Kusini.

 

Oliver pia ni baba wa watoto watano na wajukuu wawili, wawili hao pia ni wanamuziki. Ana dada zake wanne na kaka mmoja ambaye tayari amekwisha fariki. Anafurahia kuogelea katika bwawa lake la kuogelea (swimming pool) ambalo lina umbo la gitaa. Oliver ametoa zaidi ya albamu 40 na amepata kushinda tuzo nyingi mno na hata zingine hawezi kuzikumbuka.

Albamu alizotoa

  • 1978 Ndipeiwo Zano (Re-released 2000)
  • 1979 Chokwadi Chichabuda
  • 1979 Muroi Ndiani?
  • 1980 Africa (Re-released 2000)
  • 1981 Shanje
  • 1981 Pfambi
  • 1982 Maungira
  • 1982 Please Ndapota
  • 1983 Nzara
  • 1983 Oliver’s Greatest Hits
  • 1984 Hwema Handirase
  • 1985 Mhaka
  • 1986 Gona
  • 1986 Zvauya Sei?
  • 1987 Wawona
  • 1988 Nyanga Yenzou
  • 1988 Strange, Isn’t It?
  • 1988 Sugar Pie
  • 1989 Grandpa Story
  • 1990 Chikonzi
  • 1990 Pss Pss Hallo!
  • 1990 Shoko
  • 1991 Mutorwa
  • 1992 Rombe
  • 1992 Rumbidzai Jehova
  • 1992 Neria Soundtrack
  • 1993 Son of Africa
  • 1994 Ziwere MuKobenhavn
  • 1995 Was My Child
  • 1995 The Other Side: Live in Switzerland
  • 1997 Ndega Zvangu (Re-released 2001)
  • 1998 Dzangu Dziye
  • 1999 Tuku Music
  • 2000 Paivepo
  • 2001 Neria
  • 2001 Bvuma (Tolerance)
  • 2002 Shanda sountrack
  • 2002 Vhunze Moto
  • 2003 Shanda
  • 2003 Tsivo (Revenge)
  • 2004 Greatest Hits Tuku Years
  • 2004 Mtukudzi Collection 1991-1997
  • 2004 Mtukudzi Collection 1984-1991
  • 2005 Nhava
  • 2006 Wonai
  • 2007 Tsimba Itsoka

Filamu alizoshiriki

  • Jit (mwong. Michael Raeburn , 1990)
  • Neria (mwong. Goodwin Mawuru, imetungwa na Tsitsi Dangarembga, 1993). Mtukudzi ndiyo alikuwa nyota wa filamu na yeye ndiye aliotengeneza nyimbo ya filamu.
  • Shanda (mwong. John na Louise Riber, 2002, rev. 2004)

Tuzo

  • Tuzo ya KORA kwa ajili ya matayarisho mazuri ya nyimbo yake ya Ndakuwara mnamo mwaka wa 2002
  • Tuzo ya National Arts Merit (NAMA) mnamo mwaka wa 2002 na 2004 kama kundi bora la muziki/ mwanamuziki bora wa kiume
  • Tuzo ya KORA kama mwanamuziki bora wa kiume wa Africa na tuzo ya Lifetime Achievement mnamo mwezi Agosti wa mwaka wa 2003
  • Tuzo ya Reel kama lugha bora ya Kiafrica mnamo wamaka wa 2003
  • An honorary degree from the University of Zimbabwe in Desemba 2003
  • Tuzo za M-Net Best kama nyimbo bora ya filamu mnamo 1992, kwa ajili ya filamu ya Neria.

Oliver Mtukudzi – Tuku Music (Full Album)

Comments are closed.