The House of Favourite Newspapers

Tari Yawashauri Wakulima Wa Mpunga Kutumia Technolojia Ya Shadidi

0

Kutokana na uwepo wa Changamoto ya Mabadiliko ya tabia nchi, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imewasisitiza wakulima wa zao la mpunga nchini kutumia teknolojia ya kilimo shadidi kwenye zao hilo ili kukabiliana na Mabadiliko hayo pamoja na kuzalisha kwa tija.

Akizungumza na wakulima pamoja na Maafisa ugani Katika Skimu ya Umwagiliaji ya Maliwanda Wilayani Bunda Mkoani Mara Mtafiti Uchumi na Jinsia kutoka TARI Dkt. Theodore Kessy amesema ili wakulima wa zao la mpunga nchini waweze kukabiliana na Changamoto hiyo wanashauliwa kutumia teknolojia ya kilimo Shadidi.

Dkt. Kessy ameongeza kuwa Kilimo shadidi kwenye zao la mpunga ni teknologia ambayo upandikizwa miche michanga yenye umri kuanzia siku 8 hadi 14, hupandwa mche mmoja kwenye shimo, kwa nafasi pana sentimeta 25 kwa 25 na mkulima utakiwa kufanya palizi kwa kutumia vipalizi umwagiliaji wa kulowesha na kukausha shamba, pamoja na kuweka mbolea.

Amesema kuwa teknolojia hiyo ni Muhimu kwani Mkulima analazimika kulima eneo dogo lakini ana uwezo wa kuvuna mazao mengi ikiwa atafuata kanuni zote zinazotakiwa “ Kwenye hekari Moja mkulima anaweza vuna wastani wa mpaka Tani 10 hi ni sawa na tani 4 kwenye ekari moja ya mpunga”

Naye Mtafiti na Mgunduzi kutoka TARI Dkt. Juliana Mwakasendo amebainisha kuwa teknologia ya Kilimo Shadidi ni tofauti sana na kilimo cha kawaida, kwani hakihitaji maji mengi, ambapo ameeleza Mkulima atatakiwa kuweka maji kwenye shamba lake pale tu itakapohitajika kuwekwa maji.

Leave A Reply