The House of Favourite Newspapers

TASWIRA YA MSIBA NYUMBANI KWA MAMA WA ERIC SHIGONGO – PICHAZ

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global GroupEric James Shigongo (wa nne kushoto) akiwa na ndugu, jamaa, marafiki waombolezaji wengine msibani nyumbani kwa marehemu mama yake, Mikocheni, Dar.
NDUGU, jamaa na marafiki wamefika kuungana na waombolezaji na wafiwa wote nyumbani kwa marehemu Mama mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global GroupEric James Shigongo, Bi. Asteria Kahabi Kapela aliyefariki dunia leo.
Mkurugenzi wa Global Publishers, Marsha Bukumbi ambaye ni mtoto wa marehemu (anayenong’onezwa), Mahriri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (wa kwanza kushoto) wakiwa na wanafamilia na waombolezaji wengine.

 

Bi. Kapela amefariki dunia alfajiri ya leo IjumaaJulai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya KikweteMuhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Shigongo akifarijiwa na waombolezaji waliofika nyumbani kwao.
Msiba huo upo nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mikocheni B jijini Dar es Salaam ambako taratibu zote za mazishi zitafanyika.

Kwa niaba ya wafanyakazi wa Makampuni ya Global Group, tunapenda kutoa pole kwa familia ya Shigongo, pole kwa ndugu jamaa na marafiki, pole kwa wafanyakazi wenzetu kwa kupata pigo la kuondokewa na mpendwa wetu.
Wanafamilia na ndugu wengine wakiomboleza kifo cha Bi. Asteria Kapela.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe, AMEN!

 

Mkurugenzi wa Global Publishers, Lydia James Bukumbi (wa nne kulia) akiomboleza kifo cha mama yake mzazi pamoja na wanafamilia wengine.

 

YALIYOJILI: Msiba wa Mama wa Eric Shigongo

Watoto wa kike wa marehemu wakiomboleza.

 

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akizungumza jambo wakati wa maombolezo hayo.

 

Ndugu na marafiki wakimfariji Shigongo.

 

Picha na Musa Mateja | Global Publishers.

TANZIA: Mama Mzazi wa Erick Shigongo Afariki Dunia

YALIYOJILI: Msiba wa Mama wa Eric Shigongo

Comments are closed.