The House of Favourite Newspapers

Tatizo la kuchelewa kupata ujauzito

0

Hii ni hali ambayo huwatokea watu walio katika malengo ya kupata mtoto lakini mwaka unapita wakitafuta bila mafanikio na wengine hutafuta zaidi ya mwaka hadi miaka wasifanikiwe.

Tatizo hili pia huongeza idadi ya watu wanaohudhuria katika kliniki za matatizo ya uzazi wakitafuta uwezekano wa kufanikiwa kupata watoto.

Wapo wengine huamua tu kwa hiari yao kusubiri kutokana na malengo, wapo wanaotumia njia ya uzazi wa mpango kutoa tofauti ya muda kati ya mtoto mmoja na mwingine lakini wanapotaka kupata mwingine huwa tatizo.

Tatizo la kupata ujauzito huongezeka kadiri umri unavyokuwa mkubwa hasa kwa mwanamke kwa hiyo ni vema wanawake wahakikishe wanapata ushauri makini katika hili. Hali hii pia ipo hata kwa wanaume ambapo kadiri umri unavyoongezeka uwezo wa kufanya tendo la ndoa hupungua na usipoangalia hutoweka lakini kutopata mtoto huhusiana na kutokuzalisha mbegu za kiume zenye ubora.

Tatizo la kutopata ujauzito kwa mwanamke au mwanaume kushindwa kumpa mwanamke mimba huitwa ugumba au ‘Infertility’. Utasa au ‘Sterility’ ni kutokuwepo kabisa uwezekano hata wakati mwingine huhitaji tiba kutokana na kasoro ulizokuwa nazo katika mfumo wako wa kizazi.

‘Primary Infertility’ mtu hana historia ya kupata ujauzito au mwanaume hana historia ya kuwahi kumpa mimba mwanamke. ‘Secondary Infertility’ ipo historia kwa yeyote.

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Hali ya ugumba inaweza kutokea kwa mmojawapo, mke au mume au wote wawili mkawa na matatizo.

Kwa mwanaume tatizo linaweza kuwa kutokuwa na nguvu za kiume, kutokuzalisha mbegu za kiume au kutoa mbegu zisizo na sifa yaani zisizoweza kumpa mwanamke mimba na mwanamke tatizo la ugumba linaweza kusababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni au kuziba mirija ya uzazi.

MATATIZO YA UGUMBA YANAVYOTOKEA
Matatizo haya tunayaweka katika makundi manne kwa ujumla lakini kundi moja ni kwa mwanaume na makundi matatu ni kwa mwanamke.

MATATIZO KWA MWANAUME
Hapa inahusisha matatizo katika mfumo wa homoni, yaani upungufu katika homoni za kiume. Matatizo mengine ni ya kimaumbile ambapo mwanaume anakuwa na kasoro ya kuziba kwa mirija ya usafirishaji mbegu au hana kabisa mirija hiyo au mbegu za uzazi hazitoki ipasavyo.

Kasoro katika uzalishaji mbegu tatizo linalosababishwa na matatizo ya kuzaliwa nayo, maambukizi sugu ya korodani yanayoambatana na maumivu ya mara kwa mara ya korodani, korodani kutokushuka yaani kutokuwa na korodani au kuwa na korodani moja, mionzi ya x-ray ya mara kwa mara, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya huathiri uzalishaji.

Kukosa uwezo wa kufanya tendo la ndoa ambapo ni kufanya tendo la ndoa bila ya kutoa manii, kukosa nguvu za kiume au kupungua hamu ya tendo la ndoa.
Itaendela wiki ijayo.

Leave A Reply