The House of Favourite Newspapers

Tatuu Zamuumbua Esha Buheti

0

ESHA BUHETHLICHA ya kula kiapo kuwa hatokuja kujichora tatuu ya aina yoyote mwilini mwake miezi kadhaa iliyopita, staa wa filamu Bongo, Esha Buheti hivi karibuni ameumbuka baada ya kunaswa akiwa na tatuu kibao mwilini mwake.

Tukio hilo lilitokea kwenye bethidei ya mwigizaji Wema Sepetu iliyofanyika katika Ukumbi wa Wema, Kijitonyama jijini Dar ambapo paparazi wetu baada ya kumfoitoa picha kadhaa mrembo huyo, alimuuliza kulikoni avunje kiapo chake, akajibu:

“Ni kweli niliapa kabisa kutokuwa nazo lakini sijui hata ni kwa nini niliamua kubadili uamuzi wangu. Nimejiandika maneno kila kona lakini hata leo ukiniuliza nilikuwa na maana gani sijui,” alisema Esha.

Leave A Reply