The House of Favourite Newspapers

TCRA Kusaka Waliowasajilia Wenzao Laini za Simu

0

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kufanya uhakiki wa laini zote za simu zilizosajiliwa ili kuondoa wale waliosajili kwa kutumia kitambulisho vya watu wengine. 

 

Pia, uhakiki huo utawahusu wale waliosajili laini zao kwa kutumia kitambulisho tofauti ambapo wote watachukuliwa hatua za kisheria.

 

Kwa waliositishiwa huduma za laini zao za simu kuanzia Januari 20, wanaweza kuendelea na utaratibu wa usajili kwa lengo la kurudisha laini hizo zilizofungwa kama zitakuwa bado zipo au kupata mpya.

 

Imesema pia kwamba kundi la kwanza waliozimiwa laini zao ni watu 656,091 ambao wana vitambulisho vya taifa au namba lakini hawajasajili laini zao.

 

Leave A Reply