The House of Favourite Newspapers

Media Day: Vyombo vya Habari Viendane na Mabadiliko ya Kiteknolojia

0
Mwakilishi wa UNDP Amon Manyama akitoa mada katika siku ya Uhuru wa vyombo vya habari mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hotel ya Malaika Hoteli jijini Mwanza.

    

Na Johnson James | GLOBAL PUBLISHERS| MWANZA

Vyombo vya habari  nchini vimetakiwa kuendana na mabadiliko ya teknolojia kama lengo la kuendana na wakati wa utoaji wa habari zake kwa wakati sambamba na kuzingatia kanuni na taratibu za maadili ya taaluma ya huduma ya vyombo vya habari hapa nchini.

Washiriki wakifuatilia mada ambazo zilikuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.

Hayo yamebainishwa kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa  Vyombo vya Habari Duniani ambayo kitaifa yanafanyika katika Ukumbi wa Malaika Beach Hotel jijini Mwanza yakijumuisha waandishi wa habari, wamiliki wa vyombo vya habari, jukwaa la wahariri (TEF),  Tanzania Media Foundation (TMF) pamoja na Umoja wa Klabu za Wanahabari Tanzania (UTPC).

Mwakilishi wa Global Publishers katika mkutano wa siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Johnson James akifatilia mkutano huo unaoendelea kwenye Ukumbi wa Malaika Hotel jijini Mwanza.

 

Akitoa mada katika jumuisho hilo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy  amesema kuwa vyombo vya habari kwa sasa vinatakiwa kubadilika ili kuendana na wakati kwa kutumia mitandao ya kijamii kwa kupeleka habari kwa jamii ikiwamo Facebook, Twitter, YouTube na Mitandao mingine ambayo pia itaongeza mapato ya tasisi hizo ikiwa ni pamoja na kutoa uhuru wa kujieleza.

“Hali ya ushindani katika upashanaji wa habari imekuwa kubwa na biashara ya huduma ya habari inaendelea kuwa  ngumu kutokana na baadhi ya mitandao ya kijamii kuripoti habari kwa wakati na kukwamisha mauzo ya magazeti na  biashara ya matangazo, hivyo ni vema wamiliki kujitahimini upya ili kubuni mbinu za kuendana na kasi hiyo”, amesema Mungy.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzania Media Fund (TMF), Ernest Sungura amesema kuwa kwa sasa Redio nyingi hapa nchini hutumia kiwango cha asilimia  52 kuandika habari za vijijini ambapo amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kutoa fursa kwa waandishi wao kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uhuru zaidi huku akiwataka waandishi wa habari wanaoandika habari za maendeleo vijijini kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa nafasi ya kutosha katika habari zao.

Kwa upande wake Antony Dialo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya sahara Media Group (SMG) ameiomba serikai kuweka kanuni za kudhibiti mipaka ya mitandao ya kijamii kama whatsap, Twiter, Isntagram ili kuweza kupata habari zinazongatia maadili ya taalum ya Habari.

Johnson James akifuatilia mkutano huo kwenye kompyuta mpakato baada ya kuambiwa watafute baadhi ya maelezo kwenye mtandao.

Leave A Reply